![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2024/04/26/nnnnnnnnnnnnnnn.jpg?itok=hnFer7K4×tamp=1714144742)
Mrakibu Paul Mselle
Wakizungumza na EATV baadhi ya wananchi wanaeleza kuwa wakati mitaani yapo mengi wanayoyaona lakini bado wamekuwa na wakihangaika kuzifikia mamlaka zinazotakiwa kuchukua hatua.
"Tunayaona mengi mtaani, Uhamiaji waje mitaani huku wafuatilie vizuri wapo wahamiji haramu mitaani" amesema Mwamfupe
Kwa upande wa Idara ya Uhamiaji Tanzania wameeleza kuwa wataendelea kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi katika kuwadhibiti wahamiaji haramu na wasafirishwaji kimagendo, huku wakiahidi kuendelea kutoa elimu zaidi kwa jamii ili kuongeza ushirikiano zaidi.
"Tutaendelea kushirikiana na wananchi na baadhi wameshakuwa na uelewa mkubwa kuhusu makosa ya kushiriki kwenye uhamiaji haramu" amesema Mrakibu Paul Mselle
Aidha Mrakibu Mselle anabainisha kuwa wengi wanaokamatwa nchini wakisafirishwa kimagende wamekuwa wakielekea kusini mwa Afrika huku sababu za kukimbia nchi zao zikiwa ni ugumu wa maisha.