
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Benjamin Kusaga
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Benjamin Kusaga ilieleza kuwa Machi 05, 2024 mtuhumiwa Dainess Paul Mwashambo 30 akiwa nyumbani kwake Kijiji cha Mashese – Ilungu aliwanywesha sumu ya kuulia magugu aina ya “Pare Force” watoto wawili na kusababisha vifo vyao muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya kwa matibabu ambapo walipoteza maisha wakiwa wanaendelea na matibabu
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni msongo wa mawazo uliosababishwa na kutuhumiwa kwa matukio ya wizi na serikali ya Kijiji cha Mashese.
Mtuhumiwa baada ya tukio hilo naye alikunywa sumu hiyo na kwa sasa anaendelea na matibabu Hospitali ya Mkoa wa Mbeya chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi huku Jeshi hilo likitoa wito kwa jamii kuwa pindi unapopatwa na tatizo suluhisho lake sio kujichukulia sheria mkononi bali ni kutafuta ushauri au kufuata sheria inavyoelekeza ili kuepuka madhara kwako na jamii inayokuzunguka.