
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania IGP Camillus Wambura
Aliyekuwa Kamanada wa Polisi Mkoa wa Singida Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Stella Mutabihirwa amepelekwa Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai kuwa Mkuu wa Kitengo cha Makosa dhidi ya Binadamu na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (SACAP) Amon Kakwale ambaye alikuwa Mkuu wa Kikosi cha kuzuia dawa za kulevya.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi (SACAP) MArtin Otieono amepelekwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma kuwa Mchambuzi wa Makosa ya Uhalifu na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACAP) Agustino Senga ambaye alikuwa Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar.
Aidha aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACAP) Issa Suleiman ameenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACAP) Nicodemus Katembo ambaye amehamishwa kwenda kuwa Afisa Mnadhimu Kamisheni ya Polisi Jamii Makao Makuu ya Polisi Dodoma.