Jumatatu , 5th Feb , 2024

Naibu Spika wa Bunge Mussa Zungu ameiomba Wizara ya Mambo ya Ndani kuweka sheria kali kwa za kuwadhibiti bodaboda na ajali za barabarani sheria ambazo zitawabana na kuwafanya wazingatie sheria za barabarani.

Naibu Spika wa Bunge Mussa Zungu

Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 5, 2024, bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

"Suala la bodaboda ni kero kubwa sana na hasa katika utumiaji wa sheria za barabara, mimi ni mtetetezi mkubwa sana wa bodaboda lakini matumizi yao kwenye barabara yanakatisha tamaa lazima muwe na mkakati maalum wa kudhibiti ajali wanazozifanya na lazima muwe na sheria kali za kuwadhibiti na hata kuwasimamisha, sababu ukienda MOI sasa hivi asilimia 90 ni vijana," amesema Naibu Spika wa Bunge