Mshambuliaji Karl Toko Ekambi
Toko Ekambi mwenye umri wa miaka 32 anayeitumikia klabu ya Al-Ettifaq ya nchini Saudi Arabia ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusema nimehuzunishwa na kutofika mbali lakini najivunia kwa uwezo wa timu yangu kwa pamoja,ukurasa wa shindano la 4 la Afcon umefungwa na mwisho wa historia yangu ndani ya Cameroon.
Karl Toko Ekambi ameitumikia timu yake ya taifa kwa kipindi cha miaka 9 kuanzia mwaka 2015 mpaka 2024 huku ameitumikia Cameroon kwenye michezo 60 na kufunga magoli 15 sambamba na kutwaa ubingwa wa Afcon 2017 nchini Gabon