
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango
Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa Kongamano la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kuelekea Miaka Mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani na Miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi lililofanyika Uwanja wa Kawawa mkoani Kigoma.
Amesema uchumi wa dunia nzima umeathiriwa na UVIKO - 19, vita baina ya mataifa pamoja athari za mabadiliko ya tabianchi ambapo uimarishaji wake sio suala la muda mfupi amewasihi vijana kuwa mstari wa mbele katika kulinda na kutetea maslahi ya Taifa pamoja na kutumia ushawishi wao kuwahimiza vijana wengine na watu wazima kuendelea kuiunga mkono CCM kwa kuwaonesha mafanikio makubwa yaliyofikiwa chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.