
Upendo Peneza
Peneza ametangaza uamuzi huo Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Dkt Emmanuel Nchimbi.
"Nimeamua kujiunga na chama hiki kutokana na muelekeo mzuri unaofanywa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT Samia Suluhu Hassan," Amesema Upendo
Aidha, Peneza amepingana na wito wa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe wa kuitisha maandamano ya kupinga muswada wa sheria za uchaguzi ambayo yamepangwa kufanyika Januari 24, mwaka huu.