Ijumaa , 29th Dec , 2023

Mganga wa kienyeji Richard Paul, mkazi wa Kihonda mkoani Morogoro, pamoja na wenzake wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumtapeli mteja wake kiasi cha shilingi milioni tano pamoja na kufanya kazi hiyo ya uganga bila kibali.

IST

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama, na kusema watuhumiwa hao walikamatwa Desemba 28, 2023, baada ya kupewa taarifa na mteja huyo aliyetapeliwa huku wakikutwa na gari aina ya IST ambayo wanaitumia katika shughuli zao za kutapeli watu.

Kwa ujumla wake jeshi hilo linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kutenda makosa mawili tofauti, likiwemo la kuwakamata watu wanne waliokuwa wanatengeneza pombe kali aina ya Smart Gin.