
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi wa mkoa wa Rwizi Samson Kasasira, Mzee Dominic Babiiha anatuhumiwa kumuua mkewe Costansio Bakasisa akitumia mundu majira ya saa 1 asubuhi jumamosi huko nyumbani kwao eneo la Kahunga.
Taarifa Zaidi zinatanabaisha kwamba wazee hao ambao ni wakulima wamekua wakiishi vyuumba tofauti tangu walipooana.
Polisi wamesema mkewe alikataa kumpa tendo la ndoa sababu alikua akijisikia vibaya, ambapo licha ya hayo bibi huyo aliendelea kulazimishwa tendo hilo ambapo aliamu kwenda kulala chumba cha wajukuu zake.
Mzee huyo aliamua kuchukua mundu na kumuamuru atoke nje ya chumba, ambapo aliingia kwenye chumba hicho na kumshambulia na mundu mfululizo huku wajukuu wakikimbia nje kuomba msaada.