Jumamosi , 16th Dec , 2023

Kiongozi wa Kuwait Emir Sheikh Nawaf al-Ahmad al-Jaber al-Sabah amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86, televisheni ya taifa ya Kuwait imetangaza.

Sheikh Nawaf aliteuliwa kuwa mfalme mwaka 2006

Sheikh huyo aliliongoza taifa hilo lenye utajiri wa mafuta kwa miaka mitatu iliyopita baada ya kuchukua madaraka kutoka kwa kaka yake wa kambo, Sheikh Sabah al-Ahmad al-Sabah.

Mwanamfalme huyo, Sheikh Mishal al-Ahmad al-Sabah, mwenye umri wa miaka 83, ametajwa kuwa mrithi wake.

Kuwait imetangaza siku 40 za maombolezo na ofisi za serikali zitafungwa kwa siku tatu."Kwa huzuni na huzuni kubwa, tunaomboleza... kifo cha Sheikh Nawaf al-Ahmad al-Sabah" taarifa iliyorushwa kwenye televisheni ya taifa imesema.

Sheikh Nawaf aliteuliwa kuwa mfalme mwaka 2006 na kuchukua nafasi ya emir mwaka 2020.Alizaliwa mwaka 1937, alikuwa mtoto wa tano wa mtawala wa zamani wa Kuwait Sheikh Ahmad al-Jaber al-Sabah.