Jumatano , 15th Nov , 2023

Afisa Mtendaji Mkuu wa Manchester United, Richard Arnold amejiuzulu nafasi hiyo na kuhitimisha miaka 16 ya Utumishi wake klabuni hapo.

Arnold alichukua nafasi hiyo kutoka Ed Woodward mnamo Februari 2022.

Kuondoka kwa Arnold kunaashiria ujio wa Mmiliki mwenza mpya wa Mashetani hao Wekundu, Sir Jim Ratcliffe ambaye anatarajiwa kufanya mapinduzi mapya klabuni hapo ikiwa ni pamoja na kumleta mbadala wa Arnold.

Man United imemteua Patrick Stewart kuchukua nafasi ya Arnold kwa muda huku klabu hiyo ikiendelea kumsaka mbadala wa kudumu.