Jumatatu , 6th Nov , 2023

Mchezaji wa zamani wa Tottenham hotspur, Real Madrid na timu ya taifa ya Wales Gareth Bale atakuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Ligi Kuu England EPL mchezo unaozikutanisha Tottenham dhidi ya Chelsea utakaochezwa majira ya saa 5:00 Usiku.

Gareth Bale atakuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa EPL leo kati ya Tottenham dhidi ya Chelsea.

Taarifa ya Spurs iliyotolewa siku ya Ijumaa ilisema Bale atakuwa mgeni wa heshima kwenye mchezo huu na baada ya kipindi cha kwanza kumaliza muda wa mapumziko ataingia eneo la kuchezea uwanjani kwa ajili ya kuwasalimia mashabiki wa timu hiyo. Bale aliichezea Tottenham jumla ya michezo 237 alifunga mabao 75 na pasi za usaidizi wa magoli (Assist) 35.

Kwenye mchezo huu Spurs huwenda ikawakosa nyota wake Destiny Udogie na Ben Davies hawa ni 50 kwa 50 kucheza lakini Ivan Perisic, Ryan Sessegnon na Manor Solomon watakosekana kabisa. Kwa Chelsea Armando Broja na Mykhailo Mudryk wapo fiti kucheza tena lakini itawakosa Trevoh Chalobah, Carney Chukwuemeka, Ben Chilwell, Wesley Fofana, Romeo Lavia na Christopher Nkunku.