![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2023/10/23/pepe.jpg?itok=yfS9U2o0×tamp=1698089973)
Miongoni mwa rekodi anazoendelea kushikilia Pele hadi hivi sasa ni rekodi ya kuwa mchezaji pekee duniani aliyewahi kushinda kombe la dunia akiwa na umri mdogo zaidi ambapo alikuwa na umri wa miaka 17 tu mnamo mwaka 1958. Na pia ndiye binadamu pekee aliyefanikiwa kushinda vikombe vitatu vya kombe la dunia alishinda mwaka 1958, 1962 na mwaka 1970.