
Mabehewa yaliyoacha njia
Ajali hiyo imetokea eneo la Kibirizi, muda mchache tu baada ya kuanza safari, ambapo baadhi ya mashuhuda ambao pia ni abiria waliokuwa wakisafiri, wameeleza hali ilivyokuwa huku wakiomba kufanyika ukaguzi kabla ya kuanza safari.
Msaidizi wa Steshebni Masta Shirika la Reli Nchini TRC mkoa wa Kigoma Evarsti Mshana, amesema hadi sasa hakuna athari zozote zilizotokea, na wanaendela na uchunguzi kujua chanzo cha ajali hiyo.