Akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari Meneja habari na mawasiliano Simba SC Ahmedy Ally amesema hii ndio michuano yenye thamani zaidi barani Afrika na hali ya kikosi inaendelea vyema na mazoezi na kila mchezaji yupo na shauku ya kufanya vizuri katika mchezo huo.
"Maandalizi haya babkubwa yanayofanyika kwenda uwanjani. Hakuna Mwanasimba anatakiwa kubaki nyumbani, hiyo siku ni kwenda uwanjani. Historia hiyo itabaki kwa vizazi na vizazi."
"Lazima tuambiane ukweli AFL ya safari hii imeshirikisha timu nane bora na Mnyama yupo kati ya timu hizo bora, AFL zijazo zitakusanva kila mtu ambavo haitakuwa na thamani sawa na hi ya kwanza."- amesema. Ahmed Ally.