Jumatatu , 16th Oct , 2023

Mkufunzi wa Hispania Luis de la Fuente amesifu kiwango cha wachezaji wake baada ya kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Ulaya 2024 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Norway mnamo Jumapili ya Oktoba 14-2023

Fuente amesema nina furaha kuona timu yangu inaendelea vizuri kwenye njia inayopendeza,kila mchezaji ana hisia nzuri za kuwepo kwenye timu pamoja na tunajenga timu nzuri kwa ajili ya siku za mbeleni.

Luis de la Fuente aliichukua nafasi ya Luis Enrique ndani ya timu ya taifa ya Uhispania baadaya kombe la kombe la dunia 2022 huku mpaka sasa timu 7 zimefuzu kwa ajili ya michuano ya Ulaya 2024 inayotaraji kufanyika nchini Ujerumani kuanzia Juni 14 mpaka Julai 14-2024.