Jumatatu , 9th Oct , 2023

Nyota wa tenisi Mpoland Iga Swiatek ameshinda taji lake la 5 kwa msimu huu baada ya kumfunga Mrusi Liudmila Samsonova anayeshika nafasi ya 22 kwa viwango vya tenisi duniani kwa Wanawake na kutwaa taji la China Open 2023.

Swiatek mwenye umri wa miaka  22 amemshinda Mrusi Liudmila Samsonova   baada ya kumfunga kwa seti 2-0 yaani 6-2 na 6-2 na kutwaa taji hilo la 5 baada ya kushinda mataji manne kabla ya  French Open, Doha, Stuttgart na Warsaw ndani ya mwaka huu.

Iga Swiatek aliisimamisha rekodi ya ushindi wa mara 16 mfululizo kwa bingwa wa US Open 2023 Mmarekani Coco Gauff kwenye hatua ya nusu fainali huku sasa anashika nafasi ya pili kwa viwango vya ubora wa tenisi kwa upande wa wanawake  duniani.