Jumatatu , 9th Oct , 2023

Zaidi ya wanawake milioni 200 duniani wamekeketwa, kati yao zaidi ya milioni 20 wamekeketwa kupitia wataalam wa afya, huku zaidi ya wanawake na wasichana milioni 50 barani Afrika wanatakiwa kulindwa ili wasikeketwe.

wembe na kisu

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Dkt Dorothy Gwajima, wakati anafungua kongamano la kamisheni ya Umoja wa Afrika lenye lengo la kushinikiza kukomesha ukeketaji kwenye jamii.

Amesema kwa kushirikiana na viongozi wa kimila, kidini, viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya jamii inaweza kuleta mabadiliko chanya.