Bao pekee la JKT Tanzania Limefungwa na Edward Songo katika kipindi cha pili cha mchezo na ushindi huu unakuwa ni kwanza kwa kikosi hicho katika michezo yake ambayo imeshuka dimbani.
Baada ya ushindi huo kikosi hicho cha JKT Tanzania kinachofundishwa na kocha Malale Hamisi kimesogea hadi nafasi ya saba kikiwa na alama zake tano katika michezo mitano ambayo imeshuka dimbani.