
Danjibga alifanya kazi na Sauti ya Nigeria (VON) kwa miaka mingi, ambapo aliripoti sana juu ya ukosefu wa usalama ulioenea katika jimbo la Zamfara.
Alitangazwa kupotea mapema Jumatatu kabla ya mwili wake kupatikana kwenye shimo nyuma ya nyumba yake.
Katika taarifa yake, VON ilisema kuwa mwandishi huyo alitekwa nyara na "magaidi", ikielezea kifo chake kama mauaji.
Muungano wa waandishi wa habari nchini Nigeria (NUJ) na mashirika mengine ya habari yamelaani mauaji ya Danjibga.Gavana wa jimbo la Zamfara Dauda Lawal ameviagiza vyombo vya usalama kuchunguza tukio hilo.
Waandishi wenzake wa habari walisema sauti ya matangazo ya Danjibga ilkua ya weledi wa hali ya juu wakati wa kazi yake ya miongo mingi kama mwandishi wa habari.