
Rais Denis Sassou Nguesso, ndiye rais wa tatu kwa muda mrefu zaidi barani Afrika, baada ya Teodoro Obiang Nguema wa Guinea ya Ikweta na Paul Biya wa Cameroon.
Hatua hiyo Inafuatia tetesi kwenye mitandao ya kijamii kwamba jeshi limekuwa likijaribu kumuondoa madarakani kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 79, ambaye kwa sasa yuko Marekani akihudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa na viongozi wengine wa dunia.
Waziri wa Habari wan chi hiyo Thierry Moungalla alichapisha kwenye X (zamani Twitter) siku ya Jumapili, akisema alitaka kuwahakikishia umma kwamba wanaweza kuendelea kufanya shughuli zao kwa utulivu na kwamba Serikali inakanusha habari hizo za uwongo.
Tovuti ya serikali pia ilichapisha taarifa ya kukanusha ripoti za jaribio la mapinduzi. Kumekuwa na wimbi la mapinduzi barani Afrika katika miezi ya hivi karibuni, hasa hivi karibuni katika nchi jirani ya Gabon, ambako jeshi lilinyakua mamlaka mwezi Agosti.
Bw Sassou Nguesso aliingia madarakani katika nchi hiyo ya Afrika ya kati inayozalisha mafuta katika mapinduzi ya kijeshi mwaka wa 1979. Alipoteza uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi nchini Kongo mwaka 1992 lakini akapata tena mamlaka mwaka 1997 baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Kiongozi huyo wa Kongo ndiye rais wa tatu kwa muda mrefu zaidi barani Afrika, baada ya Teodoro Obiang Nguema wa Guinea ya Ikweta na Paul Biya wa Cameroon.