
Treni hiyo ya kivita ambayo Kim anaitumia kwa ziara za kigeni inaonekana kuondoka Pyongyang, vyombo vya habari vya Korea Kusini vimeripoti vikimnukuu afisa wa serikali.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika mapema siku ya Jumanne.Shirika la habari la Urusi Interfax limeripoti mapema kwamba Kim anatarajiwa kuzuru "katika siku zijazo".
Iwapo mkutano huo na Putin utafanikiwa, itakuwa ni ziara ya kwanza ya kimataifa ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini katika kipindi cha zaidi ya miaka minne, na ya kwanza tangu janga la virusi vya corona.
Viongozi hao wawili huenda wakajadili uwezekano wa Korea Kaskazini kuipatia Moscow silaha za kusaidia vita vyake nchini Ukraine, afisa wa Marekani awali aliiambia BBC mshirika wa Marekani CBS.
Ziara ya mwisho ya Kim nje ya nchi ilikuwa Vladivostok mwaka 2019 kwa mkutano wake wa kwanza na Putin baada ya kuvunjika kwa mazungumzo ya Korea Kaskazini ya kuachana na silaha za nyuklia na rais wa wakati huo Donald Trump.
Kim pia alisafiri kwenda Vladivostok kwa treni mwaka 2019.