Ijumaa , 8th Sep , 2023

Moto mwingine ambao chanzo chake hakijajulikana umezuka tena katika Hifadhi ya Mlima KIlimanjaro eneo la Indonet Rongai wilayani Rombo tangu Septemba 3, 2023.

Mlima Kilimanjaro

Taarifa iliyotolewa na TANAPA imeeleza kuwa jumla ya wazimaji moto 134 walipelekwa katika eneo hilo wakiwemo askari wa maafisa wa Jeshi la Uhifadhi, Jeshi la Akiba na wananchi wa vijiji vya jirani na kwamba mpaka sasa umefanikiwa kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa.

Aidha uchunguzi wa moto huo unaendelea lakini pia shughuli za utalii zinaendelea pamoja vikosi vingine vinazidi kupelekwa ili kuhakikisha moto unadhibitiwa kwa kiasi kikubwa zaidi.