Jumatano , 23rd Aug , 2023

Katika kukabiliana na uhalifu wananchi wa Tarafa ya Mwamashimba wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza wamekamilisha kuchimba msingi wa kituo cha polisi huku wakiendelea na michango ya kuendelea na ujenzi wa kituo hicho ambacho kinatarajiwa kukamilika kwa gharama ya shilingi milioni 100.

Wananchi pamoja na Askari wakichimba msingi

Wakazi hao wameeleza kuwa hatua hiyo imekuja baada ya Tarafa hiyo yenye jumla ya Kata 6, vijiji 30 na vitongoji 223 kukosa kituo cha polisi suala linalofanya kuwepo kwa uhalifu na kuwafanya kukosa usalama. 

Akizungumza na wananchi hao Mkuu wa wilaya ya Kwimba Ng'wilabuzu Ludigija, amewapongeza kwa hatua hiyo akisema kujengwa kwa kituo hicho kutafungua fursa za uwekezaji katika maeneo hayo.