Jumamosi , 19th Aug , 2023

Kimbunga kinachopiga upepo wa kilomita 215km kwa saa kinaelekea Mexico na kusini magharibi mwa Marekani.Kimbunga hicho cha 4, kwa jina Hilary, kinatabiriwa kuwa cha kwanza kukumba eneo la Baja California, jimbo la Mexico, Jumamosi asubuhi.

Watabiri wanasema kuwa itapoteza kasi ya upepo na kuwa dhoruba ya kitropiki, ikifuatilia kaskazini-magharibi kuelekea kusini mwa California, Nevada, Arizona na Utah.

Watabiri wanasema kuwa itapoteza kasi ya upepo na kuwa dhoruba ya kitropiki, ikifuatilia kaskazini-magharibi kuelekea kusini mwa California, Nevada, Arizona na Utah.

Hii itakuwa dhoruba ya kwanza ya kitropiki kupiga California katika kipindi cha miaka 80.
Shirika la Usimamizi wa Dharura la Shirikisho (Fema) "limeweka wafanyakazi na vifaa katika eneo hilo, na wako tayari kujibu kama inavyohitajika," Rais Joe Biden alisema Ijumaa.