
Wakazi wa mtaa wa Migombani kata ya Minazi Mirefu katika manispaa ya Ilala ambao wanatakiwa kuondoka katika eneo hilo kupisha mwekezaji anayejenga bandari kavu wamemuomba Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati suala lao la kutaka walipwe fidia inayoendana na uhalisia wa nyumba zao tofauti na fedha anazotaka kuwalipa mwekezaji ambazo wananchi hao wamesema haziendani na thamani ya nyumba zao
Hatua hiyo inakuja baada ya kudai kwamba baadhi ya viongozi ambao walikabidhiwa jukumu la kuwasimamia wananchi hao ili waweze kuzungumza na mwekezaji huyo na wananchi kushindwa kulisimamia hilo
"" Tunakuombea Rais Samia atusaidie katika hili kwani viongozi ambao walikuwa wanatusimamia katika hili hawaoneshi jitihada zote na kujikuta tukiendelea kuteseka kwani hapa kuna mavumbi mengi yanayotokana na mwekezaji kuanza ujenzi wa bandari kavu'' Amesema Solomoni Mushi Mkazi wa migombani
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya kutetea haki za wananchi kwenye eneo hilo Chumu Samweli Chumu amesema kinachowakwamisha viongozi kuwasaidia wananchi hao kilipwa stahiki zao ni siasa licha ya kwamba mwekezaji anao uwezo wa kuwalipa kwa haki
""Mimi najua mwekezaji huyu si kwamba anashindwa kutulipa lakini wapo baadhi ya viongozi anashirikiana nao katika hili'' Amesema Chuma Samwel Chuma mwenyekiti kamati ya kutetea haki za wananchi mtaa wa migombani
Hata hivyo diwani wa kata ya Miti mirefu ambaye alifika kwenye eneo hilo kusikiliza kilio Cha wananchi hao Godlisen Malisa amesema mtaji wa wafanyabiashara ni fedha lakini mtaji wa wanasiasa ni watu hivyo viongozi waonyeshe ushirikiano ambao utawasaidia wananchi hao kuondokana na kero wanazozipata kwa sasa kutoka kwa mwekezaji huyo
"" Unajua hawa wananchi tunaposhindwa kuwasaidia kwa sasa na kuamua kuwaacha tu ni hatari kwani hapa walipo wanaishi kwenye mazingira hatarishi sana kiafya na usalama wa maisha yao kutokana na ujenzi huu wa bandari kavu'' Amesema Godlisen Malisa diwani wa kata ya Miti mirefu