Ijumaa , 21st Jul , 2023

Kocha Mkuu Yanga SC Miguel Gamondi amesema amekuja nchini Tanzania kuendeleza yale mazuri ambayo yaliachwa na kocha Nasserdi Nabi hivyo wanachama na wapenzi wa klabu hiyo watarajie kuona mpira mzuri na kila mchezaji akipata nafasi ya kucheza ndani ya kikosi chake.

Akizungumza na waandishi wa habari ijumaa ya Julai 21,2023 ,Uwanja wa Benjamin Mkapa ,Dar Es Salaam Kocha Gamandi amesema kuwa ana cv kubwa katika ufundishaji wa soka la Afrika na pia hadi muda bado sijapata kikosi cha kwanza.

“Nataka kila mchezaji ajipange kucheza soka la Malengo kwa kucheza soka la chini kwa kulenga kuona wakicheza pasi za chini “amesema Miguel Gamondi kocha Mkuu Yanga SC

Kwa upande wa nyota mpya wa Yanga SC Mahlatse Makudubel “Skudu” amesema hakuchagua kutumia jezi namba sita bali alichaguliwa na viongozi wa klabu yake.

“Sikuichagua namba sita ila klabu ndio imenichangulia kabla ya kutua Yanga SC sijawahi kuvaa jezi namba hiyo,nilikuwa navaa namba kumi na moja”amesema Skudu.

Kikosi cha Yanga SC kinataraji kushuka dimbani Jumamosi Julai 22, 2023 kinataraji kucheza mchezo wa kirafiki wakimataifa dhidi ya Kaizer Chief ya Afrika kusini uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa moja usiku kwenye kilele cha siku ya Mwananchi.