
Kushoto ni mwanafunzi Ester na kulia ni Mama yake mzazi
Aidha vipimo vyote vya kiafya vimefanyika na Ester hana ujauzito na hivyo ataendelea kukaa na maafisa ustawi wa jamii ili kumsaidia kumpa ushauri wa kisaikolojia arudi shule, na mwanaume huyo atasakwa mpaka akamatwe.
RC Homera ametoa rai kwa walimu wa Pandahill kupunguza kasi ya kuchapa viboko.
Jana Juni 22, 2023, Waziri Mkuu alitoa maagizo kuhakikisha mwanafunzi huyo anapatikana mara moja na baadaye mapema leo Juni 23, 2023, Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera alitoa saa 24 na kutangaza dau la milioni 5 kwa yeyote atakayefanikisha kumpata mwanafunzi huyo.
Mwanafunzi Ester Noah Mwanyilu, alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha akiwa shuleni kwao Pandahill Mei 18 mwaka huu.