
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao amesema tukio hilo lilitokea Juni 9. 2023 majira saa mbili usiku
Kamanda Abwao amesema muuguzi huyo ambaye aliingia kazini akiwa amelewa pombe alitenda kosa hilo wakati alipopangiwa zamu ya usiku ya kuhudumu wagonjwa wa nje (OPD) ndipo alipotoka na kwenda chumba cha wagonjwa wa ndani na kumbaka mama huyo mwenye ujauzito wa karibu kujifungua ambaye alikuwa anaendelea na matibabu ya ugojwa wa malaria.
Muuguzi huyo alikutwa akiwa na bomba la sindano pamoja na dawa za usingizi huku taarifa ya kitabibu ikidhibitisha kuwa alimwingilia mgonjwa huyo.
Mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakani mapema hii leo June 13,2023 kujibu tuhuma zinazomkabili baada ya upelelezi kukamilika