
Ilhali nyota wa Yanga Fiston Kalala Mayele sambamba na kiungo mshambuliaji wa Simba Mrundi Saido Ntibazonkiza wamefungana idadi ya magoli ya kufunga baada ya kila mmoja kufikisha idadi ya magoli 17 na sasa kila mchezaji atapewa kiatu cha ufungaji bora wa msimu kwa pamoja.
Upande mwingine,Mzunguko wa 30 umeshuhudia kwa klabu mbili zinazomilikiwa na Halmashauri zikienda kucheza michezo ya mtoano ya kusalia ligi kuu ambazo ni Mbeya City na KMC ambazo zitacheza kugombania kusalia ndani ya ligi kuu Tanzania Bara kwa msimu 2023-24.