Fatuma Salum Mama wa marehemu anasema, kifo cha mwanaye hakikuwa cha kawaida kwani anamfahamu kwa namna alivyomlea na si rahisi kwake kuchukua maamuzi hayo
"Sielewi nnapoambiwa mwanangu amejinyonga hakuwa na hasira na hata alipokosea nilikuwa ninamuadhibu lakini hakuwahi kufanya kitu kama hiki" Fatuma Salum, Mama mzazi wa Yusra
Aidha bibi wa mtoto huyo ameeleza hali ya mtoto huyo kabla ya kifo chake
"Siku moja kabla hajafariki alikuwa anaumwa tumbo, alisema anasikia kitu kinatoka juu kinadondoka chini" Habiba Nandoli, Bibi wa mtoto Yusra (11) aliyejinyonga Nyengedi, Lindi
Kwa mila na Desturi za watu wa mikoa ya kusini mwa Tanzania, kutohitimisha msiba wa marehemu kwa kufanya 40 ni kigezo kimojawapo kuwa familia haijaridhika na namna ndugu yao alivyofariki ambapo familia hiyo haijapanga kuhitimisha kwa kufanya shughuli hiyo ya 40
Binti huyo mwenye umri wa miaka 11 inaelezwa kuwa tarehe 17 mwezi wa 5 alishindwa kwenda shule kwa kigezo kuwa anaumwa, ambapo alifanya kazi za nyumbani na kufua nguo zake ambapo muda wa saa 5 alijinyonga kwa kutumia nguo na kufariki