Yamoto Band
Meneja wa TMK wanaume family na mkubwa wa wanawe Said Fella amesema kuwa bendi hiyo inasafiri leo sa mbili usiku ambapo vijana hao watafanya show yao kubwa itakayofanyika tarehe 21 ya Jumamosi hii wakiongozana na meneja wa bendi Tumbiso.
Fella amesema kuwa baada ya onesho hilo kubwa nchini humo bendi hiyo itakutana na raia na wadau mbalimbali wa muziki kuongeza zaidi utandawazi wa kufanya kazi na kujitangaza zaidi kimataifa.
Bendi ya Yamoto inatarajia kurudi nchini Tanzania kuanzia tarehe 2 ya mwezi Machi huku wakijiandaa kutoa kazi na kufanya maonesho yao Jijini Dar es Salaam mikoani.