
Shigela ameyasema hayo wakati kwenye maadhimisho ya siku ya shujrani kwa mlipa kodi iliyoambatana na utoaji wa vyeti kwa walipa kodi mkoani humo.
"Unafanya uzoefu wa miaka hata mitano kwamba kwenye kipengele hiki tulikadiria kukusanya kiasi hiki kutoka kwa watu wa Madini kama sehemu ya 30% ya income tax, lakini mwaka juzi tukikusanya hiki, mwaka Jana tumekusanya hiki, kwahiyo mnatafuta ratio ambayo itawasaidia kwenye kodi ili hiyo percent isiwe kubwa sana ikaleta malalamiko au ikawa ndogo sana inaonekana mmecompromise katika ukusanyaji wa kodi, tukifanya hivyo kazi yetu itakuwa nyepesi", alisema Shigela.
Kaimu kamishna wa TRA nchini anasema katika kipindincha miezi minne wamefanikiwa kukusanya mapato kwa asilimia 208.
"Katika kipindi cha mwezi Julai 2022 hadi oktoba 2022, mkoa wa Geita uliweza kukusanya shilingi bilioni 25.27 ikiwa ni ufanisi wa asilimia 208.6 dhidi ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 12.11 katika kipindi hiko ", alisema
Baadhi ya wafanyabiashara mkoani humo wameiomba TRA iendelee kutoa Elimu kwa wafanyabiashara ili kuondoa malalamiko wakati wa ukusanyaji wa kodi huku wengine wakiipongeza kwa huduma za kielektroniki.
"Tunaomba wenzetu wa TRA, waendelee kuandaa Elimu kwetu sisi wafanyabiashara ili tuendelee kuoata Elimu ya kutosha hasa ukizingatia kwamba wengi bado Elimu haijatosha, kwahiyo tuendelee kuoata Elimu ili tuweze kuwa free kulipa kodi sisi wenyewe bila kufosiwa", alisema Wambura.
"Kaka sasa hivi unaweza, ukaingia kwenye mtandao shughuli zako zote ukazituma kwa njia ya mtandao bila kusumbuka kwenda ofisi za TRA hiyo ni namna fulani wameiboresha wao kwa ajili ya ulipaji wa kodi", alisema Inyasi.