Kituo cha kutolea huduma maalum kwa pamoja kilichojengwa Sirari mpakani mwa Tanzania na Kenya
Wizara ya ushirikiano wa Afrika Mashariki imekiri kuwa ukosefu wa elimu ni moja ya changamoto kubwa kwa wananchi na wafanyabiashara nchini hatua ambayo imewafanya washindwe kutambua fursa zinapatikana katika nchi wanachama za jumuiya hiyo ya Afrika Mashariki.
Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Amantius Msole, amesema ukosefu wa elimu miongoni mwa watanzania ni moja sababu ambazo zimesababisha wafanyabiashara wengi kuingiza bidhaa kwa njia za magendo zikiwemo zile ambazo hazistahili kulipiwa kodi na ushuru mbalimbali.
Msole ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi na wafanyabiashara katika mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Sirari muda mfupi baada ya kutembelea vituo maalum ya kutolea huduma za pamoja,
Nao baadhi ya wananchi wakiwemo viongozi wa chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA,
wamesema ukosefu wa elimu kuhusu fursa zilizopo katika soko la pamoja la Afrika Mashariki kumewafanya watanzania kuwa watumwa katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo.
Tayari ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za pamoja za forodha, uhamiaji, polisi na idara nyingine za udhibiti mipakani umekamilika katika eneo la Sirari nchini Tanzania na Isibania nchini kenya lengo likiwa ni kupunguza kero kwa pande hizo mbili.