Mwenyekiti wa Chama cha wahasibu Wanawake Tanzania TAWCA, Dk. Neema Kiure akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wahasibu Duniani
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Bw. Ludovick Nduhiye amesema Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali zenye lengo la kuwajengea uwezo wakadiriaji majenzi, wasanifu majengo na wahandisi wanawake ili kuwa nasifa za kuajiriwa, kujiajiri na kuajiri wengine.
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Programu ya kuwawezesha wanawake katika masuala ya ujenzi iliyoandaliwa na taasisi ya wasanifu majengo Tanzania, (TAWAH) jijini Dar es Salaam amezungumzia umuhimu wataalam hao kufanya mazoezi ya vitendo kwa wingi ili kuwa na ujuzi na hivyo kuwawezesha wanawake kushiriki katika maendeleo ya sekta ya ujenzi nchini.
"...Serikali inatenga asilimia 30 ya Bajeti ya Ujenzi wa Barabara kwa ajili ya miradi inayotekelezwa na wanawake hivyo waongezeeni ujuzi ili waweze kunufaika na fursa hiyo," amesema Naibu Katibu Mkuu Nduhiye.