Alhamisi , 10th Nov , 2022

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Geita imewahimiza wafanyabiashara kutunza kumbukumbu za biashara zao ikiwemo kutoa risiti za manunuzi, mauzo na gharama za biashara ili kulipa kodi stahiki na pia kutekeleza matakwa ya kisheria

Afisa Elimu na Huduma kwa Mlipakodi Bw. Justine Katiti amesema hayo wakati wa semina ya kodi kwa wafanyabiashara wa kata ya Ushirombo wilayani Bukombe huku akisema wafanyabiashara wengi wamekuwa na mwitikio mdogo wa kutoa risiti hali inayosababisha kuikosesha serikali kukusanya mapato halali

Aidha Katiti anasema Wafanyabiashara wasiotoa risiti watakutana na  adhabu kulipa faini  kuanzia Tshs.3milioni hadi Tshs.4.5milioni na pia mnunuzi asipodai risiti adhabu yake ni kuanzia Tshs.30,000 hadi Tshs.1.5milioni.

Katika semina hiyo Wafanyabiashara walitahadharishwa kujiepusha na watu ambao ni matapeli wanaojifanya ni Maafisa wa TRA na kwamba inapotokea wana mashaka na watu hao, watoe taarifa mapema kwenye ofisi ya TRA iliyo karibu nao.