Alhamisi , 3rd Nov , 2022

Kampuni ya Jubilee Alliance Insurance imewataka sasa wakulima kufika na kutumia huduma zao mpya ambazo wamezianzisha wakilenga kumsaidia mkulima huku wakizindua pia huduma za bima kwa wanaofanya biashara ya utalii.

Kampuni hiyo kupitia huduma zake mbalimbali ambazo imekuwa ikizileta kwa wananchi zimetajwa kuwa msada mkubwa ambapo kwa sasa wameanzisha mfumo maalum ambao umeorodhesha msaada ambao wewe kama mteja unaweza kuuomba kupitia mfumo endapo umelipia bima kubwa.

Hata hivyo kampuni hiyo imewataka wamiliki wa vyombo vya moto bila kujali jinsia kutumia mfumo wa msaada endapo umepata dharula ukiwa barabarani ikiwemo huduma ya ulinzi,endapo umeishiwa mafuta matatizo ya betri pamoja na kuomba gari ya wagonjwa kupiti mfumo maaalum ambao umewekwa na Jubilee Alliance Insurance