Jumanne , 1st Nov , 2022

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa mgao wa maji unaoendelea jijini Dar es Salaam unatokana na ukataji miti katika mkoa wa Pwani ambao ni chanzo cha mto Ruvu unaosambaza maji yanayotumika jijini Dar, na akiagiza vizuizi vyote vilivyoweka kwenye njia za mto ruvu kuondolewa.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia ameyasema hayo leo wakati wa akifungua kongamano la mjadala wa kitaifa wa nishati safi ya kupikia huku akielekeza kuanzishwa kwa kikosi kazi kitakachokuja na mpango kazi wa pamoja kati serikali na wadau binafsi kuhusu matumizi ya Nishati sana na endelevu ya kupikia kwa taifa letu.

Aidha Rais Samia amehamasisha mikoa yote nchini kuhakikisha inapanda miti ya matunda ili kupunguza athari za ukataji miti huku akiagiza taasisi zenye watu zaidi ya 300 kuhakikisha kuhakikisha unatumia nishati safi.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati January Makamba amemshukuru Rais Samia kwa utayari wake wa kuokoa kizazi hiki na kizazi kijacho kwa kuhimiza matumizi endelevu ya nishati safi.

Wakati mjadala wa kwanza ukiongozwa na Waziri wa Nishati, Janu-ary Makamba ukiendelea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mstaafu Prof. Anna Tibaijuka akaitaka serikali kuweka mikakati ya kurahisisha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa gharama nafuu zaidi, ili wananchi waweze kumudu.