Wananchi kijiji cha Losimingori wilayani Monduli mkoani Arusha wamefunga kwa muda barabara zote zinazokwenda kwenye minara ya mawasiliano ya simu za mkononi wakizidai kampuni hizo zaidi ya bilion moja yakiwa ni malimbikizo ya kodi ya miaka nane sasa.
Wakizungumza kwa jazba katika mkutano wa kutafuta muafaka wa sakata hilo ,wananchi hao wamesema wamefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa viongozi wao wa vijiji wamekuwa wakikwepa kuwaeleza ukweli wa fedha zao .\
Hata hivyo baada ya mvutano mkali baadhi ya viongozi wa kijiji hicho walifanikiwa kuwatuliza wananchi hao na kufungua barabara hiyo huku wakitoa siku tatu za kupatiwa majibu ya kueleweka kabla hawajachukua hatua nyingine
Wakizungumzia sakata hilo wawakilishi wa makampuni hayo akiweamo mhandisi Regan Usiri pamoja na kuwaomba wananchi hao kuwa na subira ili wakati wanafuatilia madai yao wamesema wanachojua wao ni kwamba fedha hizo zimelipwa kwa taasisi ya jeshi la wananchi kwa madai kuwa ndiyo wanaomiliki eneo iliko minara hiyo maelezo ambayo yamepingwa vikali na wananchi hao .
Pamoja na mkanganyiko huo viongozi wa vijiji wameahidi kufuatilia suala hilo ngazi za juu na ili kujua ukweli na kumaliza utata huo ambao ulisababisha baadhi ya huduma kwenye minara hiyo kusimama