
Kampeni hiyo imelenga kutoa vifaa saidizi vya kufanyia kazi ikiwemo jiko la kisasa mtungi wa Gesi na vifaa vingine Ili kuhakikisha ufanisi unaongezeka katika biashara hiyo..
Akizindua kampeni hiyo meneja wa Masoko wa coca cola kwanza Victor Amosi amesema wamefanya utafiti na kubaini vijana wengi mkoa wa Dar es Salaam wamejiari katika kazi ndogo ndogo ikiwemo hii ya kuuza chips hivyo msaada huo utawasaidia wengi.
"Tumeona jitihada kubwa ambazo serikali inafanya kuwainua vijana sisis kama kampuni tukaona sasa tuje na kampeni hii maalumu ya chipsika kiajira na coke ili kuinua sasa vijana wakaanga chips kwa kuwapa vifaa kuinua biashara yao tukianza na wilaya tano za mkoa wa Dar er salaam"amesemaVictor Amos-Meneja Masoko Coca-cola kwanza.
Kampeni hiyo pia imelenga kuwapa mafuzo vijana hao 300 watakaopatikana juu ya kutunza kumbukumbu zao na taarifa za kifedha sambamba na kupewa elimu ya matumizi ya matumizi ya majiko ya gesi ya kisasa.