Askari wa usalama barabarani akimsaidia mwananchi kuvuka barabara
Hayo yameelezwa na Mrakibu Msaidizi wa Polisi Notker Kilewa ambaye ni Kaimu Mkuu wa usalama barabarani Mkoa wa Kinondoni akihimiza kuwa wataendelea kulinda usalama wa raia na mali zao, na hasa watumiaji wa vyombo vya moto.
Aidha Kamanda Notker amewakumbusha wananchi kuendelea kutii sheria za usalama barabarani bila shuruti, ili kupunguza ajali na usumbufu barabarani.