Jumatano , 28th Jan , 2015

Staa wa muziki wa nchini Uganda, Bobi Wine ameibuka na kusafisha jina lake kwa kusema kuwa, tetesi za yeye kugundua kuwa alikua analea mtoto Simon ambaye si wake bila kujua kwa miaka kadhaa sasa ni za kweli.

Msanii wa nchini Uganda Bobi Wine akiwa na mtoto Simon

Bobi wine ameelezea kuwa hili jambo halitamfanya yeye kumtenga mtoto huyo ambaye amekuwa akimtunza kama wake kwa muda wote.

Bobi Wine amesema kuwa, ataendelea kumtunza mtoto huyu kama sehemu ya familia yake kutokana na mahusiano makubwa ambayo tayari yalikwishajengeka kati yao ingawa atahitaji mama wa mtoto huyu kuomba msamaha kwa kila pande kwa kuficha ukweli juu ya ishu hii kwa miaka yote hiyo.

Taarifa za awali ziliweka wazi kuwa star huyo ameamua kukata mawasiliano pamoja na mahusiano kati yake na mtoto huyo pamoja na mama yake baada ya kugundua ukweli huu wa kushtusha, hatua ambayo ameikanusha kabisa.