Alhamisi , 8th Sep , 2022

Kundi linalojiita  dola la kiislamu (IS) tawi la Msumbuji, limekiri kuwaua watu wanne akiwemo mtawa raia wa Italia kaskazini mwa jimbo la Nampula , shambulizi ambalo lilifanyika jumanne wiki hii.

Kundi hilo limethibitisha kupitia mtandao wake wa kijamii tawi la Msumbiji.  Vyombo vya habari nchini humo viliropoti siku ya jana kwamba mtawa huyo raia wa Italia mwenye umri wa miaka 83  aliyejulikana kwa jina la Sister Maria De Coppi, alipigwa risasi na kupoteza maisha wakati vikosi vya kijihadi vilipovamia kijiji cha  Chipene katika wilaya ya Memba .

Katika shambulizi hilo watu kadhaa wanaripotiwa kuchinjwa na vikosi hivyo. 

Katika madai yao IS wamesema kwamba wameamua kumuua sister huyo sababu anaeneza sana dini  maeneo hayo.

Vikosi hivyo pia vilichoma moto kanisa , magari mawili pamoja na mali zingine zilizokuwepo kwenye eneo hilo.

Nje  ya tukio hilo, kundi hilo la IS limekiri kuhusika na tukio ambalo lililofanyika mwezi  June mwaka huu huko  Nampula katika kijiji cha Memba na kuwachinja watu.

Eneo la Nampula linapatikana kusini mwa  jimbo la  Cabo Delgado ambapo shuguli za IS zinasemekana kuchukua hatamu. Rais wa Msumbuji   Filipe Nyusi amethibitsiah uwepo wa matukio hayo.