
Rai hiyo imetolewa na Waziri mkuu mstaafu Mizengo Kayanza Pinda mara baada ya kupokea wageni wawekezaji raia wa China wanaoishi Marekani ambao wamefika nchini na kueleza nia yao ya kuwekeza katika sekta za kilimo,utalii,ujenzi wa hotel na kumbi za kisasa,utengenezaji dawa za binadamu, kilimo pamoja na filamu
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi kituo cha uwekezaji nchini TIC amesema maeneo tajwa ambayo wageni hao wameyabainisha ni maeneo muhimu katika uchumi ukilinganisha lengo la watalii milioni tano kwa mwaka huitaji pia maeneo muhimu kwa maraddhi hivyo ujenzi wa hoteli za kisasa utaimarisha zaidi sekta hiyo.
Kadhalika na hilo kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara wachina inchini Tanzania bw ZUU amewataka watanzania wanaotaka kuagiza bidhaa china kupitia katika chemba yao ili kupata bidhaa kwa uhakika na kuepuka matapeli ambao huchafua soko.
Pamoja na hayo wito imetolewa Kwa Watanzania Kuendelea kuitunza amani Kwa kuwa imekuwa kivutio kikubwa Kwa wawekezaji kutokana kupata utulivu wa mitaji inayowekezwa.