Kesi hiyo ya ubakaji namba 33 ya mwaka 2022 imesikilizwa na hakimu Juma Mpuya na inaelezwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti akiwa nyumbani kwake mwezi Januari na Februaari mwaka huu baada ya mtoto huyo kutoka kwa mama yake eneo la Buhongwa na kwenda wa baba yake wa kambo maeneo ya Mkolani aliko kuwa akiishi na mwanamke mwingine
Maelezo ya upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali Gati Mathayo na mwendesha mashtaka Lupyana Mahenge uliokuwa na mashahidi 6 akiwemo muathirika, ambaye alieleza ilipofika usiku akiwa na watoto wenzake mshtakiwa alimwambia akale kwenye nyumba ndogo tofauti na walio lala wenzake ndipo na baadae baba huyo akaingia ndani kumbaka na kitendo hicho kilikuwa kikijirudia
Mama mzazi wa mtoto huyo alipomfuata aliambiwa na jirani wa familia hiyo kuwa mtoto wake alibakwa baada ya mke wa mshtakiwa kupeleka malalamiko katika serikali ya mtaa ndipo akamuhoji mtoto wake ambaye alikiri na taratibu za polisi na vipimo kufanyika .
Wakati wa kesi mshtakiwa alijitetea mwenyewe na hakuwasilisha shahidi yeyote ambapo alisema hajafanya kitendo hicho na kuhoji siku husika ambazo binti huyo alikaa kwake pia juu ya vipimo kufanyika pasipo kuhusisha mpelelezi wa kesi hiyo.
Kufuatia utetezi huo mahakama imemkuta na hatia na alipoambiwa kujitetea mshtakiwa akasema ana tegemewa na wazazi wake na watoto wake hivyo mahakama impunguzie adhabu
Hakimu Mpuya baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili alisema mahakama hiyo amesema wakati mshtakiwa anatenda kosa hilo alijua ana wazazi na watotto wanao mtegemea na ametenda kitendo kibaya zaidi ya mnyama hivyo anamuhumu kwenda jela maisha.