
Rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo dos Santos
Rais huyo wa zamani alifariki dunia ijumaa iliyopita katika jiji la Barcelona nchini Uhispania ambapo alienda kwa lengo la matibabu.
Mtoto wa kike wa Rais huyo Tchize dos Santos ndiye alieomba uhgunguzi wa mwili wa baba yake ufanyike.
Mtoto huyo anasadiki kwamba huenda baba yake ameuawa kutokana na kile kilichoonekana kuwa kumzuia asiunge mkono upinzani wa nchini Angola kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Wanasheria wa familia ya Marehemu Dos Santos wamesema kuwa serikali ya nchi hiyo haitakiwi kuurejesha mwili huo Angola kwa ajili ya maziko ya kitaifa kama ilivyotangaza badala yake ifuate wosia wa marehemu aliyetaka kuzikwa tena kwenye usiri wa familia nchini Uhispania.
Dos Santos alikua Rais wa Angola kwa karibia miaka 40 mpaka mwaka 2017.