
kikosi cha Simba kikiwa mazoezin leo.
Baada ya ushindi wa bao moja tuliopata katika uwanja wa nyumbani Jumapili, jana wachezaji walipewa mapumziko na leo kikosi kimeanza mazoezi na kuingia kambini moja kwa moja.
''Tumeanza mazoezi mapema kwa kuwa lengo letu ni kuhakikisha tunapata matokeo mazuri ugenini ili kufuzu hatua ya nusu fainali''amesema Ahmedy Ally.
Kwa upande mwingine Meneja huyo wa mawasiliano wa Simba amesema morali ya wachezaji ipo juu na hakuna aliyepata majeraha makubwa katika mchezo wetu wa kwanza tunamuomba Mungu waendelee kuwa salama mpaka katika mechi yetu ya marudiano.