Jumatatu , 11th Apr , 2022

Wanasiasa wa ngazi za juu nchini Uganda wameitwa Polisi ili kuthibitisha madai waliyotoa kwamba, aliyekua spika wa bunge la nchi hiyo marehemu Jacob Oulanyah alilishwa sumu jambo lililopelekea kifo chake.

Wanasiasa mashuhuri nchini Uganda akiwemo  Robert Kyagulanyi maarufu kama Bob Wine   wameitwa Polisi kwa kutoa madai hayo kwamba  Jacob Oulanyah amekufa kwa sumu. 

Msemaji wa polisi nchini Fred Enanga amesema kuwa walioitwa polisi ni pamoja na Makamu mwenyekiti wa chama cha upinzani cha  NRM Godfrey Kiwanda, Mbunge Santa Okot na  Gilbert Olanya 

 ‘’Wanatakiwa watueleze kwa ushahidi jinsi spika alivyolishwa sumu bila kutia shaka yoyote, kwamba nani alimlisha sumu, sumu ilipatikana wapi, na namna yoyote ile inayoonesha marehemu alilishwa sumu.’ Amesema Enanga wakati akizungumza katika makao makuu ya jeshi hilo huko Kampala nchini Uganda.

 “Kwa mujibu wa rekodi za afya tulizonazo, hakukua na sumu kwenye damu yake . sasa tunataka wao waje kututhibitishia’’

Siku ya jana,   Bw. Kyagulanyi maarufu kama Bob Wine ambaye pia alihudhuria maziko  aliitaka serikali kufanya uchunguzi wa kutosha juu ya madai ya sumu iliyosababisha kifo cha spika huyo.