Jumatatu , 12th Jan , 2015

Chama cha Mapinduzi Wilayani Butiama kimesema kuwa hakitakuwa tayari kukubali manyanyaso katika maeneo ya migodi mkoani Mara, na kiko tayar kufanya maandao endapo serikali haitarekebisha dosari zilizopo

Wachimbaji katika mgodi wa Katarya mkoani Mara

Chama hicho  kimesema hakitakuwa  tayari kuruhusu  wazara  ya nishati  na  madini kuwatumia baadhi  ya  watu  kwa  ajili  ya kuwaondoa  wachimbaji  wadogo   wa  madini katika  mgodi   wa  Katarya  huku  kikipanga kufanya  maandamano  makubwa  kama  moja  ya  hatua  ya kupinga unyanyasaji huo unaodaiwa  kufanywa  na serikali kupitia wizara  hiyo  ya  nishati na madini.

Wakizungumza  na  wachimbaji hao  wadogo   katika  kijiji  cha  Kataryo  halmashauri  ya  Musoma  wilayani  Butiama   viongozi   wakuu  wa  chama  hicho katika   wilaya   ya  Butiama  wamesema  kuwa  wizara  hiyo  ya  nishati na  madini imekuwa  ikitumia serikali  na  vyombo  vya  dola  wilayani  humo  kwa lengo  la  kutaka kuwanyang’anya  wachimbaji  maeneo hayo  kinyume  na  maelekezo  ya  ilani  ya CCM
 
Kwa upande  wake  mbunge wa jimbo  la  Musoma vijijini Nimrod mkono, akizungumza na  maelefu  ya  wachimbaji  hao  amesema  kitendo hicho  kinachofanywa  na wizara hiyo ya  nishati  na madini kutumia  serikali  na  vyombo  vya dola  wilayani  Butiama  kuwaondoa   wananchi  hao  kisha kugawa  maeneo hayo  kwa   watu  ambao  amedai  ni mawakala  wizara  hiyo  kamwe   hakitakubalika.

Tangu  wananchi hao  wagundue  kuwapo  kwa  madini  katika  eneo  hilo, serikali  kupitia kwa  mkuu  wa  wilaya  ya  Butiama ilifika na  kuufunga mgodi  huo  hatua ambayo ilisababisha  kamati  ya siasa  ya  CCM  wilaya  ya  Butiama  kukutana na  kutoa  tamko  la kuufungua  mgodi huo  ili  kuwezesha  vijana  hao  kuendelea na  shughuli zao  za uchimbaji  wa  madini.