Jumanne , 5th Apr , 2022

Bei za mafuta zitakazoanza kutumika kuanzia kesho Aprili 6, 2022 zimepanda.

Gari ikiwekewa mafuta kwenye kituo cha mafuta

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Mhandisi Godfrey Chibulunje, ametangaza mabadiliko hayo leo Aprili 5, 2022.

Kwa upande wa mafuta ya Petroli lita moja itakuwa ikiuzwa 2,861 wakati Dizeli itauzwa 2,692 kwa lita.

Aidha Mhandisi Godfrey Chibulunje amesema mafuta ya taa lita moja itauzwa 2,682.